Takribani miaka 30 iliyopita,Pico Iyer alisafiri kwenda Japan, akaipenda nchi na akahamia huko. Mfwatiliaji wa karibu wa roho ya binadamu, Iyer anasema kwamba sasa anaona anajua machache kuhusiana na Japan -- au, hakika, kuhusu chochote kile -- kama ambavyo alidhani anajua miongo mitatu iliyopita. Kwenye hii tafakari ya kishairi kuhusu hekima, Iyer anaelezea kuhusu uelewa unavyokuja na umri: kadri tunavyodhani tunajua, ndivyo tunagundua tunajua kidogo.
