Usitaabike na msongo wa mawazo katika ukimya.
Kuwa na hisia si dalili ya udhaifu -- humaanisha kwamba sisi ni binadamu, anasema mtayarishaji vipindi na mwanaharakati Nikki Webber Allen. Hata baada ya kugundulika na ugonjwa wa msongo wa mawazo na hofu, alijisikia aibu kumwambia mtu yoyote, aliweka hali yake katika usiri mpaka pale msiba wa mtu wa karibu katika familia yake ulipotokea, kutokana na hali kama yake. Katika mjadala huu muhimu kuhusu afya ya akili, anaongelea wazi kuhusu hangaiko lake -- na kwanini jamii ya watu wasio wazungu ina ulazimu wa kuondokana na unyanyapaa ambao huepelekea watu kuwaza msongo wa mawazo ni udhaifu na kuwatenga walio na hangaiko hilo katika kupata msaada.
