Masimulizi ya Majora Carter kuhusu ustawi mpya wa miji
Katika mhadhara uliojaa hisia, mwanaharakati mshindi wa tuzo ya MacArthur, Majora Carter anaelezea kuhusu mapambano yake kutetea haki za kimazingira huko Bronx Kusini -- na anaonyesha namna ambavyo maeneo ya miji waishiko wanyonge wachache yanaathirika kutokana na sera mbovu za mipango ya miji.
